Maafisa wa polisi kutoka Kituo cha Polisi cha Lumakanda, Kaunti ya Kakamega, wakifanyia kazi taarifa kutoka kwa umma, mapema leo wamezuia gari lililokuwa likishukiwa kusafirisha mmea wa cannabis sativa (bangi).
Maafisa hao waliweka mtego wa kimkakati kando ya Barabara Kuu ya Webuye–Eldoret, hatua iliyopelekea kunaswa kwa gari hilo lililokuwa likitokea Busia kuelekea Eldoret.
Baada ya upekuzi kufanyika, marobota mawili yalipatikana ndani ya gari hilo. Kila robota lilikuwa na uzito wa takriban kilogramu 10, likiwa na mmea mkavu unaoshukiwa kuwa ni bangi.
Dereva wa gari hilo alikamatwa papo hapo na gari husika kuzuiliwa kituoni huku uchunguzi zaidi ukiendelea.
